SHALOOM NICE ANIMATION HEADER

Tuesday, March 17, 2015

THE NIGHT OF GLORYThe night of Glory , ni  Mkesha unafanyika kila Ijumaa ya pili ya au ya mwisho mwezi, Mkesha huu ni wa kusifu na kuabu  na maombi na maombezi . Katika mkesha huu watu kutoka katika madhehebu mbalimbali wanakutana ili kumlilia Mungu katika mambo mbalimbali ya mtu binafsi na yale ya kitaifa.

Mkesha wa The night of Glory mwezi huu utafanyika siku ya ijumaa ya tarehe 20/03/2015  kuanzia saa  2 ; 00 usiku katika kanisa la
 KKKT  USHARIKA  WA  KARIAKOO.
Mkesha huu pia utakuwa unarushwa LIVE na redio Upendo FM, sanjari na hivyo mkesha utapambwa na waimbaji mbalimbali  wakiongozwa na Morning glory Praise team ya kariakoo.

USIPANGE KUKOSA KUFIKA KATIKA MKESHA HUU WA KUSIFU NA KUABUDU  

Monday, March 16, 2015

NAFASI YA MWANAMKE KIBIBLIA


MWANAMKE ni mwanadamu mwenye jinsia ya kike, ambaye pia Mungu amempa uwezo  wa kubeba mimba na kuzaa, ndani yake analo tumbo la uzazi .
 "Apataye Mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA.  MITHALI 18:22
Kuna mambo matatu hapa yametajwa. Kwanza ni Mtu, pili ni Kitu Tatu ni Kibali, sasa haya mambo ma tatu yaliyotajwa kila moja lina faida yake na pia linahusiana na kitu kinacho fanana, Kwanza nimesema ametajwa mtu kwasabu Mke siyo kitu hapana bali mke ni Mtu, ambaye ndani yake kuna kitu na ndani ya hicho kitu kuna kibali sasa nitaanza kuzungumzia Mtu.


Maandiko yanasema APATAYE mke sasa hili neno APATAYE linatosha sana kufahamisha ubora wa mke mwema kwasabu hii inamaanisha kwamba alitafuta kwasabu hakuna kupata pasipo kutafuta Yesu alisema TAFUTENI NANYI MTAONA Sasa kumbe ili kuona ambako ndiyo huleta kupata hakuji pasipo kutafuta maana huwezi kupata amabcho hujakiona na huwezi kukiona ambacho hujakitafuta, Sasa mke mwema anatafutwa kwa bidii na kwa nguvu na kwa imani hii inamaanisha ya kwamba mke ni mtu mwenye thani kubwa sana kupita mali na vyoote alivyonavyo mtu sasa mke ni Mtu mke siyo kitu kwa hivyo basi kupata mke ni kupata mtu siyo kupata kitu no bali ni kumpata mtu ambaye ndani ya huyo mtu ndimo kunahicho kitu, sasa hili ni la kwanza kumpata mtu sasa kama utamchukua mkeo kwa mtazamo huu kwamba yeye ni mtu na siyo kitu basi utapata majibu ya kwamba ananafasi kubwa ya kuwa mshauri mkubwa na pia kuwa wakwanza kujua mabo yako yote pasipo kumficha,

KUPATA KITU

Kama nalivyosema mke siyo kitu bali mke ni mtu lakini ndani yake ndipo kuna kitu sasa hiki kitu hakitaonekana endapo huyu mwanamke hatapewa nafasi anastahili kupewa ndani ya ndoa yake unajua huwezi kutoa kitu kama hujapokelewa yani hujakubaliwa ndiyimaana imendikwa kwamba Wote WALIOMPOKEA ALIWAPA uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu YOHANA 1:12, Hapa tunaona ya kwamba Yesu aliikuja nakitu lakini kile kitu hakukitoa kwa mtu ambaye hajampokea bali alikitoa tu kwa mtu ambaye amempokea yani amemkubali na kumpa nafasi yake ndiyo maana utaona wale ambao wamempa Yesu nafasi hawateswi na Majini wala Magonjwa maana Kuna kitu Yesu amewapa kutokana na wao kumpa nafasi.


 Ndivyo ilivyo kwa mke mke anapoingia kwenye ndoa huwa anakuja na kitu na kile kitu kitaonekana tu pale anapopewe nafasi yake aikalie yeye kama mama wa familia lakini endapo atabanwa na kunyimwa nafasi oooh ni mbaya sana maana itakuwa hasara, wanaume wengi leo wamepata hasara kwasabu ya kuwadharau wake zao, ni muhimu kufahamu kwamba Mungu aliyesema kwamba kuna kitu ndani ya mwanamke ni Mungu mtakatifu na mwenye nguvu na mwenye thamani sasa kama Mungu ni Mtakatifu ni Mwenyenguvu na pia anathamani isiyopimika basi uwena uhakika kwamba kila asemacho na cho ni kitakatifu kina nguvu na chathamani sasa kwakuwa amesema kwamaba apataye mke apata kitu chema basi uwe na uhakika kwamba hicho kitu ni kitakatifu, kina nguvu na chathamani sasa kama huyu mama atanyanyswa na mume basi mume huyo atakuwa ni MPUMBAVU NAMBA MOJA DUNIANI ambaye kwa kutokujua anajikoseha kitu kitakatifu chenye nguvu na pia cha thamani, ok sasa ndani ya Mwanamke kuna macho ya kumuona Shetani nakujua madhara yatakayotukia ukisoma kitabu cha mwanzo utagundua wakwanza kumuona Shetani alikuwa ni Hawa na siyo Adamu pia ukisoma kitabu cha Esta utagundua kwamba Yule Hamani alikufa kwasabu tu ya kuuupuuza ushauri mzuri wa mkewe alipommwambia Achana na Mordekai maana hutamuweza, lakini hamani akapuuza ushauri huo akaendelea kushindana na Mordekai matokeo yake Hamani akauawa kifo cha aibu yeye pamoja na familia yake yote ukisoma kitabu chote cha Esta utaziona habari hizo, Hata habari za Abigaili aleyemponya mumewe asiangamizwe na Daudi Huy Nabali alimkosea Daudi na Daudi akapanga kumwangamiza kabisa lakini mkewe hakuyajua hayo maana Nabali alimficha mkewe hakutaka ajue lakini Mfanyakazi wao mmoja ndiye akamwambia mkewe Nabali kuhu kosa alilolifanya Mumewe na hapo ndipo Agaili akamwendea Daudi kumwomba Msamaha na hii akaokoa Familia isingamizwe kwa upanga wa Daudi hii titufundishe kwamba kumficha mke na kuto kumpa nafasi yake ni mbaya sana kwasabu yeye huwa anaona mampema sana hatari ijayo ni sawa na Abigaili alishajua kwamba sasa tunaenda kufa lakini Mumewe hakuliona hilo alifikiri ni amani tu 1SAMWELI 25:14-35. Nahiki ndicho kitu cha thamani kilichomo ndani ya mke mwema.

KUJIPATIA KIBALI KWA BWANA

Siku moja nilitoa mfano wa max (wastani wa asilimia) nilipokua nikisema na vijana wenye wachumba halali pale BOKO basihaya.
Max ambazo Mungu anampa mtu mwenye mke na max anazompa mtu bachela ni tofauti, nikaseama ya kwama Mtu bachela Mungu anamtazama kwa matazo wa max50 na mtu mwanandoa Mungu anamtazama kwa max 100 kwasabu siku ile apomaliza kuumba voyote Akasema tazama ni vyema sana yani aliipatia kazi yake max 100 baada ya kuipima MWANZO 1:31, lakini alipomuumba Admu peke yake kbla ya kumpatia mke aliipima kazi yake akaipa max 50 kwa kusema SIVEMA mtu huyu awe peke yake MWANZO 2:18. Hii inaonyeshwa kwamba Mungu mwenyewe kwa kinywa chake ANAIKOSOA kazi yake na kusema Sinjema pamoja nakuweko kilaaina ya mnyama na madini na mafuta na Mwanaume kuwepo duniani lakini bado Mungu anasema sivema sasa kama kwa kuwapo vitu vyoote hivi bado Mungu anaseama SIVEMA basi uwe na uhakika ya kwamba hicho kimoja akilichokosekana ni chamuhimu kuliko vyote ambavyo tayari vipo, yani mke ni bora kuliko Mali zoote Pesa Madini na Mafuta havifikii thamani ya mke wanaume wapumbavu huwa wanheshimu na kujali mali zao kupita wake zao huo ni UPUMBVU MKUBWA na kikukosa hekima ya Mungu na nikuongozwa na roho ya Shetani. hivyo Mungu alimheshimu mwana mwanamke kwakufanya kuwa bora kupita vyote sasa anyemdharu mkewe basi anamdharau Mungu na Uumbaji wake,

Baada ya Mungu kupatia Adamu mke ndipo Mungu Akaipima kazi yake na kuipa max zote100 na hapo ndipo akamwambia Akawabariki na kuwambia TAWALENI.MWANZO 1:27-28. Hii inaonesha ya kwamba hakuna baraka ya mtu moja bli walibarikiwa wote wawili Mke na Mume pia Mungu hakuikabidhi dunia kwa Bachela no bali aliikabidhi dunia kwa Wanandoa kwasabu kabla ya adamu kupata mke hakuambiwa katawale no bali aliambiwa tawaleni hii ni baada ya Kupata mke maana yake ni kwamba MUNGU HAMWAMINI BACHELA BALI HUMWAMINI MWENYE MKE MWEMA na ndiyo sababu kiongozi wa Kabisa Mungu anampima kupitia ndoa yake ndiyomaana nasema kama mtu ameshindwa kuitunza nyumba yake hawezi kulitunza kanisa, hii ikufunulie kwamba Kibali cha Mungu Humjia mwanamuwe baada ya kupata mke, ndipo anasema Apataye mke apata kitu chema tena hujipatia kibali kwa BWANA,

Note;  Mke mwema si yule anaye jua maombi, na kufunga tuu, bali pia anajituma katika kutafuta mzigo (fedha/ anaongeza kipato cha mume mwema na familia).
Amen

Na. Mwl. Noel Tenga


Shalom! Shalom! Shalom!

Wapendwa wa Mungu, wasomaji wa ukurasa huu wa blog ya Shalom nice, naomba nichukue nafasi hii kuwasalimu na kuwatakie heri ya mwaka  mpya 2015. Nikweli kwa kipindi kirefu sasa katika ukurasa kumekuwa kuna kimya cha muda mrefu sana, naomba nichukue nafasi hii kuwaomba radhi kushindwa kuwapa habari mbalimbali kama nilivyokuwa nikifanya mara zote.


Mara nyingi mahali ambapo palikua na ukimya wa muda mrefu ujue kunajambo kubwa na zuri  la kimaendeleo linaandaliwa. Katika kipindi chote hicho nimekuwa na muda mzuri wa kutafakari ni jinsi gani tunaweza kuboresha namna ya kupata habari za matukio mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi kwa wakati na tukakufikishia wewe msomaji wa blog hii.
Hivyo kwa sasa team ya Shalom Nice imejipanga kuhakikisha tunakuletea habari na matukio mbalimbali. Tumejipanga katika habari za kijamii bila kusahau kutoka katika msingi au sera yetu ya kulitangaza jina BWANA  na kusema matendo makuu ya JEHOVA  ya kila siku.Napenda  kuchukua nafasi hii kuwakaribisha  wasomaji  na wapenzi  wa blog hii kwa upya kabisa na kuwahakikishia tunajali maoni yenu na tunaendelea kuyafanyia kazi  kilasiku inayoitwa leo.

Saturday, March 29, 2014

UPENDO KILAHIRO ANAKUKARIBISHA KESHO

Mwimbaji maarufu wa muziki wa injili nchini tanzania Upendo Kilahiro akishirikiana na mume wake Amon Kilahiro anakukaribisha siku ya kesho katika tamasha la kusifu na kumwabudu Mungu
Atasindikizwa na waimbaji kama vile Christina Shusho,The Voice,Gloria Kilahiro,The Reapers na wengine wengi

Upendo Kilahiro
Tamasha hilo litafanyika katika kanisa la Victory Christian Centre (VCCT) lililoko Mbezi Beach kuanzia saa nane mchana bila kukosa karibuni nyote

MIAKA 30 YA NDOA YA MWALIMU CHRISTOPHER NA DIANA MWAKASEGE

Watumishi wa Mungu Mwalimu Christopher na Diana Mwakasege wiki iliyopita walimshukuru Mungu na kusherehekea miaka 30 ya ndoa yao huko jijini Arusha


Sherehe hizo zilihudhuriwa pia na mkuu wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania KKKT Askofu Dr Alex Malasusa pamoja na ndugu na jamaa wa karibu wa familia ya Mwalimu Mwakasege
Mungu aendelee kuwainua watumishi hawa ambao wanafanya kazi ya kulisha kondoo zake

PICHA KWA HISANI YA GK

Friday, March 14, 2014

REBECCA MALOPE KUPAMBA TAMASHA LA PASAKA

Mwimbaji maarufu au malikia wa muziki wa injili nchini Africa ya Kusini Rebecca Malope kwa mara nyingine tena atalipamba tamasha la pasaka kwa mwaka huu
Rebecca
Tamasha hili pia litapambwa na waimbaji wengine kama Ephraim Sekeleti kutoka Zambia, Upendo Kilahiro, Upendo Nkone, Rose Muhando na wengine wengi
Upendo Kilahiro

Rose Muhando


Ephraim Sekeleti
Tamasha la mwaka huu litabeba kaulimbiu ya TANZANIA KWANZA HAKI HUINUA TAIFA ambapo tamasha hili litazinduliwa rasmi April 20 mwaka huu litakuwa linatimiza miaka 14 tangu kuasisiwa kwake na Msama PromotionsMonday, March 10, 2014

MAADHIMISHO YA MIAKA SABA YA HOCET SIKU YA JANA

Siku ya jana kituo cha kulelea watoto yatima cha Hananasifu Orphange center (HOCET)
kilitimiza miaka saba tangu kuanzishwa kwake amabapo watu mbalimbali walifika kituoni hapo kuungana na watoto hao katika sherehe hizo ambazo zilifanyika katika kituo hicho kilichoko Mkuranga Mkoa wa Pwani

wakati wa kwenda utelezi ulikuwepo kutokana na mvua zinazoendelea kunyeshawatoto wa HOCET wakichoma nyama ibada ikiendelea

shuhuda


praise team ya watoto

kwaya kutoka Tabata

maombezi kwa watoto

igizo
 mtumishi wa Mungu Samson Zani kutoka KKKT usharika wa Segerea akisema jambo
 kamati ya kushughulika na kuhakikisha kuwa kituo kinapata usafiri

 watu wakipata chakula kilichoandaliwa na watoto hawa

 mradi wa kuku na hawa ni baadhi tuu wapo wengi sana kwa sasa zaidi ya 1000
 mkurugenzi wa HOCET ndugu Hezekia Mwalugaja akiteta jambo na mtumishi Zani

marafiki ndugu na jamaa kama tunavyojua dini iliyo safi ni kuwasaidia yatima na wajane hivyo basi kama umeguswa na kituo hiki unakaribishwa sana kikitembelea hata mawazo yako pia yanawezakuwa ni asset kwa kituo hiki ambacho kimelenga sana kujitegemea kuliko kuomba misaada na kwa sasa hakina mfadhili wa aina yoyote na kina miradi mbalimbali kama vile kuku zaidi ya 1000 kwa sasa,ng'ombe 17 kwa sasa mashine ya kutotolesha vifaranga 2000 kwa wakati mmoja mboga mboga nk
kwa wewe uliyeguswa na kituo hiki unaweza kukichangia chochote kile ambacho Mungu atakuongoza kupitia Account namba 01J1021421500 HANANASIF ORPHANAGE CENTRE CRDB  au mawasiliano 0784396560 na 0713261425 uliza chochote kuhusu HOCET kupitia namba hizo au kama una msaada wowote